Jumatano , 26th Feb , 2020

Msanii wa HipHop hapa nchini Nay Wa Mitego amefunguka na kusema hana dini yoyote wala kabila kwenye maisha yake, bali ana imani tofauti kwenye kumuamini Mungu vile anavyojua mwenyewe.

Picha ya msanii Nay Wa Mitego

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Nay Wa Mitego amesema hakuna mahali popote wanaposema kama utafuatili dini utaenda mbinguni.

"Imani yangu ni ya tofauti sana, sina dini wala kabila kwanza dini itakupeleka wapi, hakuna sehemu iliyoandikwa kwamba itakupeleka mbinguni, halafu tuamini katika dini gani sasa Uislam au Ukristo na ipi ndiyo sahihi, mimi naamini katika imani yangu ya Mungu hata vitabu vya dini vimeandika hivyo" amesema Nay Wa Mitego.