"Ninaolewa kweli" – Tunda

Jumatatu , 11th Mar , 2019

Video Vixen maarufu katika mitandao ya kijamii, Tunda, amefunguka juu ya pete aliyopost hivi karibuni, na kusema kwamba pete hiyo amevishwa na mchumba wake, ambaye anatarajia kufunga naye ndoa.

Akizungumza na www.eatv.tv, Tunda amesema pete hiyo akutarajia kwa kuwa ilikuwa ni 'suprise', hivyo watu wakae mkao wa kula kushuhudia harusi yake na mpenzi wake huyo ambaye hajataka kumtaja.

“Ni pete ya uchumba, ilikuwa suprise mwenyewe nilikuwa sifahamu, mahari bado na wala sijui itakuwa ni bei gani, ndo naolewa kweli wasubiri tu waone ndoa ndani ya mwaka huu inshallah”, amesema Tunda.

Msichana huyo ambaye aliwahi kuwa kwenye mahusiano na rapper Young D, amesema kwamba kwa sasa ameamua kubadilika na kutulia, ili aweze kumudu ndoa yake.