"Sisi 'wabongo' tunapimana mafanikio" - Wakazi

Ijumaa , 28th Jun , 2019

Nguli wa muziki wa Hip Hop nchini, Webiro Wassira maarufu kama 'Wakazi', amezungumzia tabia ya watu kufuatilia maisha ya wengine na kuyapima kwa muonekano wa nje tofauti na uhalisia.

Wakazi

Amesema hayo katika kipindi cha DADAZ cha EATV, alipokuwa akielezea historia ya maisha aliyokulia kwa wazazi wake na jinsi alivyokuwa akitatishwa tamaa kuwa hatoweza kufanikiwa kirahisi katika kazi yake.

"Mimi nimekulia katika mazingira magumu, hatukukua kwenye maisha ya kusema 'I love you', tumelelewa kijeshijeshi sana ndio maana niko kigumu lakini sio kwa sababu nafanya hip hop", amesema.

"Kibongo bongo au Kiafrika tunapimana mafanikio kutokana na vitu ambavyo tunaviamini kuwa ndiyo mafanikio yenyewe, mfano kuwa na nyumba, gari, kuoa au kuolewa. Unakuta mtu anaweza kukwambia moja kwa moja na mwingine hatokwambia, mwingine anakwambia 'we si umesomea kitu fulani kwanini usifanye'?, wakati anajua mimi ninafanya muziki", ameongeza Wakazi.

"Lakini mimi naelewa kwa sababu nimeishi kwenye nchi za ulimwengu wa kwanza, unakuta mtu hakuulizi unamiliki nini, una mpenzi au la, bali atakuuliza 'are you happy?'".

Mtazame hapa akizungumza zaidi.