Tiba ya Saratani kugunduliwa

Jumapili , 7th Apr , 2019

Kundi la wanasayansi wa Israel, wameahidi kuwa wapo katika mchakato mzito wa kuleta tumaini jipya juu ya kupatikana kwa tiba ya saratani ndani ya mwaka mmoja.

Dkt. Illan Morad ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Accelerated Bioevolution Biotechnologies inayoshughulikia masuala ya Biotechnology, anatengeneza kitu kinachoitwa MuTaTo, ambayo licha ya kuwa na jina baya kama ilivyoelezwa, lakini inatarajiwa kuja kurudisha uzima wa watu wengi walioathirika na saratani

MuTaTo ambayo ni muunganiko wa 'peptides' ambazo zimelenga moja kwa moja seli za saratani kwa sumu kali ilizonazo na kuziua.

“Tiba yetu ya saratani itaanza kufanya kazi kuanzia siku ya kwanza, itadumu kwa wiki na haitakuwa na madhara yoyote kwa binadamu, na itakuwa nafuu sana kuliko matibabu ya sasa ambayo yana gharama zaidi”, amesema Dkt. Morad  akiliambia jarida la New York Post.

Dkt. Morad ameendelea kusema kwamba baada ya kutumia mchanganyiko huo walioutengeneza kwa panya mwenye vimelea vya saratani, ilileta matokeo mazuri baada ya kuua vimelea hivyo vya saratani bila kumuathiri panya, na kwamba wale waliowahi kupitia tiba ya mionzi ni kwa jinsi gani wataelewa kuwa hii ni 'big deal'

Takriban watu milioni 18.1 kila mwaka wanagundulika kuwa na saratani duniani, na iwapo MuTaTo itafanya kazi, itakuwa ni habari njema ulimwenguni kote.

 

 

Source: Distractfy