Twitter yazuia kupost kwa njia ya SMS

Alhamisi , 5th Sep , 2019

Ikiwa zimepita siku chache tangu akaunti ya mwanzilishi pia mkurugenzi mkuu wa Twitter Jack Dorsey kudukuliwa, sasa mtandao huo umeamua kufanya mabadiliko kadhaa ili kuongeza ulinzi zaidi kwa watumiaji wake.

Twitter wamesema kwa sasa wanaondoa uwezo wa mtu kuweza 'ku-tweet' kupitia njia ya ujumbe mfupi ambayo ili ifanye kazi lazima uunganishe namba yako ya simu na akaunti yako ya Twitter.

Inaelezwa kuwa, njia iliyotumiwa na wadukuzi kudukua akaunti ya Jack Dorsey ni namba yake ya simu na wadukuzi hao walianza kutuma ujumbe kadhaa katika akaunti yake bila kuingia katika akaunti kwa njia zilizozoeleka kama tovuti au 'application' maalum ya Twitter.

Twitter walipojulisha umma kuhusu mabadiliko hayo.

Mpango huo una dhumuni la kuifanyia marekebisho zaidi ili kuleta usalama ila hawajasema lini watairudisha tena lakini wachunguzi wa masuala ya teknolojia wanaona huenda wakaleta uwezo wa kuhakiki mara mbili zaidi (Two factor authetication), kupitia uwezo huo wa namba japo bado haiwezi kuwa ndiyo tiba ya usalama moja kwa moja.