Jumanne , 2nd Oct , 2018

Watafiti kutoka chuo kikuu cha madawa cha Stanford huko nchini Marekani, wamegundua kuwa urefu ni moja ya sababu kubwa zinazoweza kusababisha ugonjwa wa 'varicose vein'.

Mtu mwenye ugonjwa wa varicose vein

Mmoja wa madaktari wa chuo hicho ambaye ni mtaalamu wa masuala hayo Dr. Nicholas Leeper, amesema “hatukupata tu uhusiano kati ya urefu na mishipa ya varicose, lakini tafiti za maumbile zimeonyesha genetics na urefu pia husababisha 'varicose vein', amesema Dkt. Leeper.

Ugonjwa huu wa 'varicose vein' huathiri mishipa ya damu na kupekea kuvimba na kujikunja kunja kwa mishipa ya damu, na kuifanya kuwa ya rangi ya zambarau. mara nyingi huwapata watu wanene, wajawazito, wanaosimama hedhi, wenye umri zaidi ya miaka 50, na pia kusimama muda mrefu.

Chanzo kikubwa cha ugonjwa huu ni pale damu inaposhindwa kutembea vizuri mwilini na kusababisha kujaa mahali, na hatimaye kuvimba na kuanza kuwasha.

Athari zake kubwa huweza mpelekea mtu kufanyiwa upasuaji wa kurekebisha mishipa ya damu (vein) pale damu inapoganda (blood cloting), kuvuja damu kwani muda mwengine hupelekea kupasuka, miguu kuvimba, kumletea muwasho na kumfanya asiwe huru,.