Wananchi waokota pesa barabarani

Ijumaa , 14th Dec , 2018

Gari maalum la kubeba pesa nchini Marekani limeleta baraka kwa wakazi wa mji wa New jersey, baada ya kupata hitilafu kwenye milango yake na kusababisha baadhi ya pesa hizo kumwagika.

Kupitia video moja katika mtandao wa Twitter, inaonesha wakazi mbali mbali waliokuwa njiani wakishuka kwenye magari yao na kuokota pesa hizo, kitendo ambacho kimesababisha ajali ndogo ndogo za barabarani kwa mujibu wa polisi wa kitongoji cha East Rutherford katika mji huo.
 

Kampuni ya magari hayo ya kubebea pesa inayojulikana kama 'Brinks', imethibitisha kuwepo kwa tukio hilo,  lakini wameshindwa kujua ni kiasi gani cha pesa kilichopotea.