Jumanne , 19th Mar , 2019

Imekuwa ikiaminika kwamba Sayansi ina maibu ya kila kitu, hasa kwenye masuala ya kidunia, na ndio maana leo hii mgonjwa anaweza pasuliwa akafanyiwa oparesheni na akapona.

Lakini sayansi hii hii inayoaminiwa, bado kuna baadhi ya mambo imekosa majibu mpaka sasa. Ukiachia kushindwa kuzuia kifo kutokea kwa kiumbe hai, lakini pia kuna mambo mpaka leo imeshindwa kupatia majibu baadhi ya mambo ambayo yapo duniani na yenye kushangaza.

Hapa nakuletea vitu vitano ambavyo mpaka sasa sayansi ambayo inafanywa na wanasayansi waliobobea, imeshindwa kupata majibu imekuwaje, imetokeaje, au utakuwaje.
 

1. Mwanga wa Hessdalen (The Hessdalen Lights)

 

 

 

Kwa miongo sasa tangu kuripotiwa kwa mara ya kwanza mwaka 1930, watu wnaaoishi katika bonde la Hessdalen nchini Norway, wamekuwa wakishuhudia mwanga wa ajabu ukipita angani, mwanga huu umekuwa ukitokea muda wowote, usiku, mchana, asubuhi, na kucheza cheza huku ukibadilisha rangi.

Tangu mwaka 1983 wanasayansi kutoka sehemu mbali mbali wamekuwa wakifanya utafiti wao, kujua nii hasa chanzo cha mwanga huo, lakini mpaka sasa hawajapata majibu sahihi juu ya chanzo chake.

2. Viduara vya ajavu vya Namibia (The Fairy Circle Of Namibia)

Huko Namibia kuna sehemu moja imeingia kwenye maajabu haya, sehemu hii ni ardhi yenye majani, lakini cha ajabu, ina viduara vingi ambayo kati kati yake hapaoti kitu chochote, duara hizi huwa za ukubwa tofauti tofauti. Wanasayansi walishachukua mchanga na kufanya utafiti kwa nini hali hiyo imetokea, lakini mpaka sasa hawajapata majibu kwa nini imetokea, na kubaki kuwa ni siri yake Mungu mwenyewe.

      3.The Taos Hum

Hii hata jina la moja kwa moja la Kiswahili imekuwa ngumu kulipata, ila huko nchini Mexico katika mji wa Taos, wakazi wake wamekuwa wakipata shida na kelele za ajabu. Kelele hizo ni kama zile zinazosikika pindi zinapochomekwa nyaya za kwenye runinga, yaani pindi waya wa sauti unapochomekwa kwenye sehenu ya waya wa picha. Sauti hizo zimekuwa kero kubwa mpaka wengine kufikia hatua ya kupata magonjwa ya akili.

Tangu mwaka 1990 serikali imeshindwa kupata jibu sahihi ni nini hasa kinachosababisha, na mpaka sasa wanasayansi nao hajapata majibu.

4. The Devils Kettle In Minnesota

Haya ni maajabu mengine yaliyopo nchini Marekani katika jimbo la Minesotta, ambapo kuna water fall imepewa jina la 'Devils kettle', maporomoko haya ya maajabu yana sehemu mbili za kumwaga maji, sehemu ya kwanza, maji yake yanakwenda katika mto blue, lakini mengine yanaaagukia kwenye shimo lililopo kwenye miamba, lakini cha ajabu maji hayo hupotelea hapo, bila kujua yanaelekea wapi. Wanasayansi wamefanya uchunguzi wao kuangalia huenda kuna sehemu yanatiririkia lakini hawajagundua kitu chochote mpaka sasa, na kubaki kuwa tatizo lililokosa ufumbuzi.

5. The Sleep Epidemic Of Kazakhstan

Katika nchi ya Kazkhastan kwenye mji wa Kalachi, kuna mahali kijiji kizima huugua ugonjwa wa ajabu, mamia ya watu hupoteza fahamu na kulala kwa masaa. Hali hii imetokea kwa mamia ya miaka mpaka sasa, wananchi wa eneo hilo hupoteza fahamu ghafla na kulala, kisha wakiamka huonekana  kama wamerukwa na akili lakini baadaye hukaa sawa.

Wanasanysi walipofanya utafiti, walihisi ni kutokana na migodi iliyopo karibu yao, lakini baada ya utafiti kukamilika, tatizo hilo halikuhusiana hata kidogo na shughuli za migodini, na kusababisha mamia ya watu kuanza kukikimbia kijij hicho.

Lakini hivi karibu wameanza kupata majibu mengine ingwa mpaka sasa hayajawapa majibu ya moja kwa moja kuwa hicho ndicho chanzo, baada ya kugundua kuwa maradhi hayo yametokana na hewa ya carbon monoxide na  hydrocarbons zinazozalishwa kwenye shughuli za migodi, na kutaka wanakijiji kuhama kabisa eneo hilo, ingawa na lenyewe lipo kwenye uangalizi kama kweli ndio chanzo sahihi cha tatizo hilo.