Wanaume watakiwa kuwalipa mishahara wake zao

Jumamosi , 9th Mar , 2019

Mhubiri mmoja kutoka nchini Ghana, Ekow Badu Wood amewataka wanaume wote ulimwenguni kuwalipa mshahara wanawake wao kwa ajili ya kazi wanazozifanya nyumbani.

Picha ikiwaonesha wanandoa wakiafrika.

Kwa mujibu wa mhubiri huyo wanawake hutekeleza majukumu mengi nyumbani na kuhakikisha wanadumisha amani katika jamii hivyo ni vyema kuwalipa mshahara kila mwezi ili kuwapa motisha ya kuboresha nyumba zao zaidi.

"Njia moja ya kutoa shukrani kwa wanawake ni kuwalipa mshahara kila mwezi, hii ni kwa ajili ya kazi ambazo hufanya ili kuboresha ndoa zao, malipo hayo yatawafanya wawe na motisha zaidi," amesema mhubiri huyo.

Mhubiri huyo amesisitiza kuwa kila familia hunawiri panapo mwanamke na hivyo wanapaswa kutambulika na kutuzwa.