Washindi wa Nogesha Mahaba wapatikana

Alhamisi , 13th Feb , 2020

Kampeni ya Nogesha Mahaba ya iliyoandaliwa na East Africa Radio imefanikiwa kuwapata washindi wanne wa kampeni hiyo, ambao wataenda kusheherekea siku ya wapendanao "Valentine Day" Zanzibar, Kilimanjaro na Arusha.

Balozi wa kampeni ya Nogesha Mahaba kutoka East Afrika Radio Lesa Sidi kushoto, na Meneja Masoko wa Precision Air wakimkabidhi tiketi mmoja wa washindi wa kampeni hiyo

Orodha ya washindi hao ni Ramadhani Haruna na mpenzi wake Mwanaisha Ramadhani ambao watakwenda mkoani Kilimanjaro na kufikia katika Hotel ya Kilimanjaro Wonders.

Mshindi wa pili ni Yusuph Zuberi, atakwenda na mpenzi wake Bansa Michael mkoani Arusha na kufikia Two Mountains Lodge.

Washindi ambao wote watakwenda visiwani Zanzibar na kufikia katika hoteli ya Zanzibar Bahari Villas ni Joseph Enock na mpenzi wake Latifa Frank pamoja na Juma Mathias na mpenzi wake Hailat Juma.

Safari hizo zitaanza siku ya kesho Februari 14 na kurudi Februari 16, 2020 na usafiri ni bure kabisa chini ya Shirika la Ndege la Precision Air.