Jumapili , 16th Jun , 2019

Idadi ya matukio ya ulawiti watoto imeongezeka kutoka 12 hadi 533 kutoka mwaka 2017 hadi Juni 2018 kutokana na kupungua kwa nafasi ya wazazi katika kuwalinda watoto.

Ulawiti watoto

Hayo yamebainishwa na wadau kutoka TGNP Mtandao katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Jijini Dar es Salaam.

TGNP imesema kuwa suala la usalama wa mtoto linatakiwa kuangaliwa kwa ukaribu zaidi kutokana na kuwapo matukio mengi ya ukatili kwa watoto yakiwemo ya ulawiti.

Tarehe 16 Juni ya kila mwaka ni siku ya 'Mtoto wa Afrika', siku maalum ambayo inakumbukwa kutokana na jinsi ambavyo watoto wa shule wa Kiafrika waliuawa kikatili na makaburu eneo la Soweto nchini Afrika Kusini wakipinga unyanyasaji uliokuwa ukiendelea.

Tukio hilo lilitokea mnamo Juni 16, 1976, ambapo inakadiriwa kuwa zaidi ya waandamanaji 20,000 walihusika, huku makadirio yakiwa ni zaidi ya wanafunzi 176 hadi 700 inatajwa kuwa walipoteza maisha.