Whatsapp, Facebook na Instagram zatoweka kwa muda

Jumapili , 14th Apr , 2019

Mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram na Whatsapp imetoweka hewani kwa muda na mmiliki wa mitandao hiyo hajatoa taarifa yoyote kwa watumiaji wake mpaka sasa.

Nembo za mitandao hiyo

Mitandao hiyo inayomilikiwa na Mark Zuckerberg, imebaki ikitumika kutuma ujumbe tu kwa ule wa Whatsapp bila kumfikia mlengwa na kwa upande wa Facebook na Instagram zenyewe hazifunguki kabisa.

Siku kadhaa nyuma mitandao hiyo imepost kwenye kurasa zao za twitter ikionesha namna ilivyoboresha huduma zao. Tukio hilo la kutoweka kwa mitandao hiyo sio mara ya kwanza kutokea.

Siku kadhaa zilizopita mmiliki wa mitandao hiyo aliziomba serikali zote ulimwenguni kutengeneza sheria za kusimamia mitandao, ili kuepusha athari mbaya zinaonekana kwenye jamii kutokana na watu wachache wasio na maadili.