Ijumaa , 14th Feb , 2020

Taarifa mpya ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp  zinasema, umefikisha idadi ya watumiaji Bilioni 2 duniani kote ambapo mwishoni mwaka 2017 waliripoti kuwa unawatumiaji Bilioni 1.5 .

Picha ya mtandao wa Whatsapp

Mtandao huo umeongeza jumla ya watumiaji Milioni 500 kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita na ulianza kufanya kazi mwaka 2009, kisha ukanunuliwa na kampuni ya mtandao wa Facebook mwaka 2014 chini ya tajiri  Mark Zuckerberg.

Mtandao huo wa WhatsApp ulinunuliwa kwa Tsh Trilioni 43, na kufanya kuwa mtandao na chombo cha habari kilichonunuliwa kwa bei kubwa zaidi ila mtandao wa Facebook ndiyo unaongoza kuwa na watumiaji wengi zaidi ikiwa na idadi ya watumiaji Bilioni2.5.

Aidha kiongozi wa mtandao huo wa WhatsApp Will Cathcart, amesema wanakamilisha mpango wa kutunza na kuficha siri binafsi za mtumiaji wa mtandao huo

"Katika historia yote ya binadamu watu wanatakiwa wawasiliane kwa njia ya siri na  binafsi kwa kila mtu, hatufikirii kuendelea hivyo katika jamii hii ya kisasa" amesema Cathcart.