Zari awafungukia Watanzania

Jumatatu , 11th Mar , 2019

Mfanyabiashara kutoka Uganda ambaye kwa sasa makazi yake ni nchini Afrika Kusini, Zarina Hassan, 'ZaritheBosslady', amefunguka juu ya wanaomuita mshamba baada ya kupost picha akiogelea nyumbani kwake.

Zarina Hassan.

Mwanamama huyo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa instagram ameandika kuwa aachwe na maisha yake, kwani kama wakiona hawawezi kutazama picha zake basi waondoke katika mtandao huo.

"Sijawahi ona mtu anaogelea na dera, sijui ni mimi tu au?. Mniache na ushamba wangu wa Kiganda na nyie mbaki na ujanja wa Kibongo, na mtaendelea kuona picha zangu za hivi kila wikiendi kwani haya ni maisha yangu", ameandika Zari.

Zari ameamua kuandika hivyo baada ya kuibuka mijadala mtandaoni kuhusu picha zake hizo alizoweka jana Jumapili akiwa ameonekana kuvalia mavazi ya ufukweni.