Jumatano , 26th Sep , 2018

Uchumi wa nchi yoyote duniani hutegemea masuala mbalimbali lakini moja kati ya masuala hayo ni miundombinu imara na ya kutosha. Kwa mujibu wa taarifa ya World Economic Forum nchi zinazoongoza kwa kuwa na miundombinu bora duniani ni pamoja na Hongkong, Singapore, Uholanzi-

Marekani, Japan na nyinginezo.

Siku za hivi karibuni hapa nchini tumeshuhudia kuanza kutumika kwa barabara za juu maeneo ya Tazara ijulikanayo kwa jina la Mfugale flyover na kupunguza foleni kwa kiasi kikubwa, inadaiwa daraja hilo litaokoa takribani shillingi za Kitanzania bilioni 400 kwa mwezi.

Mradi huo umegharimu shilingi bilioni 95 za Kitanzania ikiwa ni moja ya mipango ya serikali katika kujenga na kuboresha miradi mbalimbali nchini na kuijenga Tanzania ya viwanda. Ikiwa flyover nyingine tayari imeshaanza kujengwa maeneo ya Ubungo

www.eatv.tv leo tunakuletea flyover tano kubwa zaidi duniani kwa mujibu wa World Economic Forum.

5.Spagetti flyover,Uingereza

Hii ipo katika jiji la Birmingham, jina halisi la flyover hii ni Gravely Hill Interchange iliyofunguliwa rasmi May, 24,1972. Jina la flyover hii limetokana na mwandishi wa habari wa gazeti la Birmingham Mail, Roys Smith aliyefananisha muonekano wa daraja hilo na chakula aina ya Tambi. Daraja hilo limechukua takribani miaka 4 kumalizika linatajwa kuwa na gharama ya Paundi milioni 10 sawa na shilingi bilioni 30 za Tanzania.

4.Judge Harry Pregerson, Marekani

Flyover hii ipo Los Angles Marekani,yenye njia tano, lilifunguliwa rasmi 1993, lina futi 130 kutoka ardhini. Daraja hili lililopewa jina kwa aliyekuwa hakimu wa serikali Harry Pregerson,liligharimu dola za kimarekani milioni 135 sawa na shilingi bilioni 324 za Tanzania.

3.Nampu flyover, China.

Hili linapatikana jijini Shanghai,China. linathamani ya dola za kimarekani milioni 259 sawa ni bilioni 621.6 za Tanzania ni flyover yenye njia tatu.

2.Springfield flyover, Marekani

Hili linapatikana Virginia nchini Marekani, takribani magari 430,000 hupita kila siku huku likitajwa kuwa ni daraja linalotumiwa sana kuliko madaraja yote nchini .lilianza kutumika mwaka 1960, lenye thamani ya dola milioni 276 sawa shilingi trilioni 1.6 za Tanzania.

1.Marquette flyover,Marekani

Hili ni la kwanza duniani lilianza kujengwa mwaka 2004 na kuanza kutumika rasmi 2008, lina thamani ya dola za kimarekani milioni 810 sawa na shillingi tilioni 1.9 za Tanzania

Hizi ni baadhi ya flyover zenge gharama kubwa zaidi duniani zinazosadikiwa kuwa na mchango mkubwa katika kujenga uchumi wa nchi zao.