Jumatano , 3rd Oct , 2018

Mtandao wa kijamii unaopendwa na wengi, instagram, umepata hitilafu ambapo watumiaji wake wanashindwa kufungua.

Tatizo hilo limetokea sehemu mbali mbali duniani, ikiwemo nchi za Afrika, Ulaya na Australia, na kuwakosesha raha ya mtandao huo watumiaji wake ambao wako zaidi ya milioni 800 hapa duniani.

Tanzania ni moja ya nchi iliyoathirika na tatizo hilo ambapo watumiaji wa instagram wameshindwa kuingia kwenye mtandao huo na kufanya chochote.

Mpaka sasa wamiliki wa mtandao huo hawajatoa taarifa yoyote juu ya hitilafu hiyo iliyojitokeza, ambayo sio mara ya kwanza kutokea, na haijajulikana kama utaridi ama la. 

Hata hivyo baada ya dakika 40, mtandao huo ulirejea kufanya kazi kama kawaida.