Jumatatu , 18th Feb , 2019

Kuelekea mchezo wa kombe kongwe zaidi nchini England na pengine duniani kwa ujumla (FA Cup), kati ya wenyeji Chelsea dhidi ya Manchester United, Man United wanakabiliwa na deni la kulipa mbele ya Chelsea.

Kushoto ni Ole Gunnar na kulia ni Mike Phelan

Timu hizo ambazo leo zinakutana kwa mara ya tano katika michuano hiyo tangu mwaka 2010, Chelsea ndio yenye matokeo mazuri zaidi ambapo imeshinda mara 3 huku Man United ikiambulia sare pekee katika michezo minne iliyopita.

Chelsea imekuwa na wakati mzuri inapokutana na Man United katika michuano hii ambapo ukiacha kushinda tu pia imefanikiwa kufunga mabao matano katika hizo mechi 4 huku Man United ikifunga mabao mawili tu.

Hata hivyo mchezo huu unaonekana kuwa na mvuto kutokana na mabadiliko ya benchi la ufundi la Man United ambapo tangu iwe chini ya Ole Gunnar Solskjær imefungwa mechi moja tu dhidi ya PSG.

Wachezaji wa Chelsea 

Pia Chelsea imekuwa haina mwendelezo mzuri kiasi cha kushuka hadi nafasi ya 6 huku Man United ikipanda hadi nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi kuu ya England.

Matokeo zilipokutana kwenye FA Cup.

May 19, 2018 FA Cup
Chelsea 1 - 0 Manchester United
Mar 13, 2017 FA Cup
Chelsea 1 - 0 Manchester United
Apr 01, 2013 FA Cup
Chelsea 1 - 0 Manchester United
Mar 10, 2013 FA Cup
Manchester United 2 - 2 Chelsea