Ijumaa , 17th Sep , 2021

Timu ya ABC inayoshiriki ligi ya kikapu jijini Dar es salaam kwa upande wa wanaume, imefanikwa kutinga hatua ya Fainali ya RBA baada ya kuifunga Ukonga Kings kwenye mchezo wa tatu kwa pointi 60-56.

Mcheza kikapu wa timu ya JKT akijaribu kuurusha mpira ili afunge na kuikusanyia alama timu yake kwenye Ligi ya kikapu ya mkoa wa Dar es Salaam 'RBA' kwa msimu wa mwaka 2021.

Ushindi wa 88-78 kwenye mchezo wa kwanza pamoja na 87-85 kwenye mchezo wa pili ilitosha kuwasogeza ABC karibu, kuelekea kunyakua ufalme wa kikapu Dar es salaam.

Vile vile kutakuwa na mchezo wa kusaka nani ataungana na ABC katika fainali hiyo ambapo JKT watachuana vikali na Savio Basketball club.

Ikumbukwe kuwa mchezaji wa Zamani wa NBA, Hasheem Thabeet anayecheza katika timu ya Savio atakuwa na kibarua kizito kuhakikisha anaisaidia timu yake kutinga fainali kwakuwa mpaka sasa wapo sare ya 1-1 na wapinzani wao kati ile michezo 5.