
African Lyon vs Stand United
Goli hilo limefungwa na mshambuliaji wake pembeni Abdallah Mguhi ‘Messi' katika dakika 23 ya kipindi cha kwanza ya mchezo na kuweza kuiandikia timu yake bao la pekee
Kufuatia ushindi huo, Afrika Lyon imeweza kupanda juu katika msimamo wa Ligi kuu mpaka kufikia nafasi ya 9 ikiwa na point 29 ambapo awali ilikuwa katika nafasi ya 13 kwa pointi 26.
Ikumbukwe kuwa Abdallah Mguhi 'Messi' ndiye aliyechungulia nyavu za timu ya Simba SC katika mzunguko wa kwanza na kutibua rekodi ya kutofungwa kwa Simba katika mzunguko huo.