Ajibu arejea Stars, kitendawili ni hiki hapa

Jumatano , 1st Mei , 2019

Mshambuliaji wa Yanga Ibrahim Ajibu, amejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 42, wa timu ya taifa ya Tanzania ambacho ni maalum kwa michuano ya AFCON 2019 pamoja na CHAN.

Ibrahim Ajibu

Kocha wa Taifa Stars Emmanuel Amunike, ametaja majina hayo leo kwenye makao makuu ya shirikisho la soka nchini (TFF), ambapo amemjumuisha kinara wa pasi za magoli kwenye ligi Ibrahim Ajibu.

Kwa mujibu wa Emmanuel Amunike kikosi hicho cha wachezaji 42 kitatumika katika michuano ya AFCON 2019 nchini Misri na CHAN nchini Cameroon.

Baada ya Ajibu kukosekana kwa muda mrefu katika kikosi hicho utata unakuja kuwa kuchaguliwa kwake na Amunike kutampa nafasi ya kucheza AFCON au CHAN.

Tanzania itakuwa nchini Misri kuanzia mwezi Juni ambako itashiriki michuano ya AFCON 2019 ikiwa imepangwa kundi C na timu za Algeria, Senegal na Kenya.