Jumatatu , 21st Mei , 2018

Nyota wa zamani wa Newcastle United Alan Shearer ambaye kwasasa ni mchambuzi wa soka, ameishauri klabu ya soka ya Chelsea kufanya kila njia kumbakiza nyota wao Eden Hazard hata kama kocha Antonio Conte ataondoka.

Shearer amesema Hazard ni mchezaji muhimu sana kama Chelsea inataka kupata mafanikio msimu ujao haina budi kumbakiza na kuongeza wachezaji wengine kwaajili ya kusaidiana naye ili kumwongezea nguvu.

''Kwa namna yoyote ile hata kama Conte ataondoka lakini Chelsea maco yao yanatakiwa kumtazama zaidi kijana wa miaka 27 Eden Hazard, bado ni hazina ya timu hivyo lazima wahakikishe haondoki'', amesema.

Klabu za Real Madrid na Manchester City zinaripotiwa kuhitaji huduma ya nyota huyo wa kimataifa wa Ubeligji ambaye leo ametajwa kwenye kikosi cha wachezaji 23 watakao kwenda Urusi kuiwakiisha nchi kwenye fainali za Kombe la Dunia mwezi Juni.

Jumamosi iliyopita Hazard aliifungia timu yake bao pekee la ushindi lililoipa ubingwa wa Kombe la chama cha soka nchini England (FA).