Alichokisema David Molinga juu ya hatma yake Yanga

Jumamosi , 1st Aug , 2020

Yafuatayo ndiyo majibu ya mshambuliaji wa Yanga, David Molinga dhidi ya David Kampista ,Mtangazaji wa kipindi cha Michezo cha Kipenga cha East Africa Radio kinachoruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 2 Usiku.

Mfungaji bora wa klabu ya Yanga msimu wa 2019/20, David Molinga (Pichani) akiwa katia Studio za East Africa Radio kwenye Kipindi cha Michezo cha Kipenga kinachoruka kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 2 Usiku

-
KUHUSU KUTOELEWANA NA MKWASA
-
"Hakuna shida yeyote kati yangu na Mkwasa, Yeye ni kama Baba yangu pale ninapokosea kama mwanaye lazima aoneshe kuwa hapa mwanangu sijapenda hivyo hakuna utofauti wowote kati yetu,Kikubwa mechi kati ya Yanga na Biashara ilikua pia ni maandalizi kuelekea dabi dhidi ya Simba,hivyo kutolewa iliniumiza sana hata kwa mchezaji yeyote anayetaka kucheza asingefurahia" - David Molinga
-
KUHUSU KUZOMEWA NA MASHABIKI
-
"Mashabiki ndio wako hivyo ukifanya vibaya watakuzomea tu kwa sababu wao wanataka ufanye vizuri na hawakuzomei kwa ubaya Kwahio mimi naichukua kama chachu ya kunifanya nifanye vizuri" Molinga
-
KUHUSU MKATABA WAKE
-
"Nimebakiza mkataba wa mwezi mmoja na Yanga, Ni kweli Timu nyingi zinanihitaji nimepokea ofa lakini nawapa kipaumbele Yanga kwa sababu ni familia yangu na nimeizoea ligi naamini msimu ujao nitafanya vizuri" Molinga

 

'Baada ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar kule kaitaba, kocha Luc Eymael aliniambia angependa kufanya kazi na mimi msimu ujao, pia Injinia Hersi Said alisema tutakaa chini kuongea zaidi, hivyo nasubiria ofa yao '' Molinga.
-
KUHUSU KUKATA PESA YA MASHABIKI
-
"Sikukataa kuchukua pesa mimi sikuiona, Hakuna mtu anakataa hela inawezakanaje ufunge na uwe na hasira mimi sikuiona ile pesa,kingine ni kuwa mkataba wangu ni kuwapa furaha mashabiki wa Yanga hivyo posho kutoka kwa mashabiki haipo katika mkataba wangu" - Molinga
-
KUHUSU MORRISON
-
"Morrison naongea nae Kama ninavyoongea na wachezaji wengine tu, Ni mchezaji mzuri sana uwanjani ila mambo yake ya nje ya Uwanja ni yake binafsi siwezi kuyazungumzia"
-
ZAHERA NI NANI KWAKO
-
"Zahera Ni Mwalimu wangu nilikutana naye kwenye Timu ya Taifa ya Congo" - Molinga
-
KUHUSU MALENGO,AHADI YA ZAHERA KUKATWA MKONO IWAPO
-
"Sijatimiza Malengo yangu Niliyojiwekea, Sijacheza mechi nyingi ni mechi 10 tu nilizomaliza dakika 90 nadhani imechangia kunifanya nisifikishe malengo yangu ambayo kwa msimu ni kumaliza kuanzia mabao 15 kwenda Mbele" - Molinga
-

MECHI ANAZOZIKUMBUKA

Mechi zitakazobaki kichwani mwangu ni dhidi ya Polisi Tanzania tuliyotoka 3-3, baada ya kuwa nyuma kwa bao 3-1,nilitokea benchi nikawawazisha mabao mawili,Mechi dhidi ya Alliance ya Mwanza,Pia dhidi ya Namungo na hata Lipuli ambayo ilikua ya mwisho kwa msimu.

 

Michezo hiyo nilikua na msongo mkubwa wa mawazo, na nilikua natolewa maneno mengi mabaya, lakini nilipopewa nafasi nilifanya vizuri,hivyo sitozisahau.

 

KUHUSU UMRI WAKE

''Nina Umri wa miaka 22'' Molinga
NENO KWA WANAYANGA
-
"Nawapenda Sana Mashabiki wa Yanga, Ukiichezea Yanga unakuwa mwanayanga, Yanga Ni kubwa Kuliko mchezaji yeyote na Hi Ni Timu ya Wananchi" Molinga