Jumanne , 11th Aug , 2020

Kocha mpya ya timu ya Juventus ambaye pia ni kiungo mchezeshaji wa zamani wa timu hiyo na timu ya Taifa la Italy anakusudia kukisuka kikosi cha Juventus vyema ili kiwe bora katika mashindano ya ubingwa wa Ulaya msimu ujao

Andreas Pirlo akiwajibika katika kikosi cha vijana cha Juventus chini ya miaka 23

Pirlo ambaye ameteuliwa majuzi kuchukua nafasi ya kocha  Maurizio Sarr aliyefutwa kazi baada ya kutolewa katika mashindano ya mabingwa na olympic lyon katika  hatua ya 16 bora

Katika kusudio lake la kuijenga timu hiyo ataanzia marekebisho kwenye idara ya  kiungo  huku akitaka kumruhusu  Aaron  Ramsey  kuondoka  na kumtafuta kiungo mwingine bora  zaidi ambapo  Tony Kroos na Isco awanatajwa moja wapo kuhamia Juvetus toka  Real Madrid

Kumekuwa na mjadala mkubwa juu ya uwezo wa Pirlo kakabidhiwa mikoba mikubwa  ya  Ukocha akiwa  hana uzoefu wa kutosha katika nafasi hiyo licha ya kuwa mchezaji mahiri wakati wake