Ijumaa , 18th Mei , 2018

Nyota wa zamani wa Arsenal Mikel Arteta, ameripotiwa kufikia makubaliano ya awali na uongozi wa Arsenal kwaajili ya kuchukua mikoba ya Arsene Wenger ambaye ameachana na klabu hiyo.

Moja ya masharti yanayosemekana kuwekwa na Arteta ni kuondolewa kwa mtalaam wa matibabu wa timu hiyo Colin Lewin kutokana na kile kilichoelezwa kuwa alishindwa kumtibu vizuri alipokuwa akichezea klabu hiyo.

Arteta ambaye ni kocha msaidizi wa Manchester City, amekuwa kocha ambaye anaongoza orodha ya makocha wanaotajwa kuwaniwa katika nafasi hiyo ambayo imeachwa na Arsene Wenger.

Man City imedai kuwa haijapata ofa yoyote kutoka Arsenal juu ya Arteta ambaye ana umri wa miaka 36 kwa kuwa bado ana mkataba klabuni hapo.