Jumanne , 18th Jun , 2019

Klabu ya Azam FC imeachana na wachezaji wake 8 ambao inaelezwa kuwa mikataba yao imemalizika hivyo hawataongeza na kuanzia sasa ni wachezaji huru.

Chirwa

Msemaji wa Klabu hiyo Jaffar Idd Maganga amesema kuwa uongozi wa juu tayari umeshafanya mazungumzo na wachezaji hao na umewapa ruhusa ya kuangalia timu nyingine.

"Uongozi umenipatia majina ya wachezaji ambao mikataba yao imemalizika na hatutaweza kuendelea nao na tatari wamepewa ruhusa ya kuweza kutafuta maisha ya soka katika timu nyingine.” - Maganga.

Aidha amewataja wachezaji hao ni nyota wa zamani wa Yanga Obrey chirwa, nyota wa zamani wa Simba Daniel Lyanga na Ramadhani Singano. Wengine ni Joseph Kimwaga, Enock Atta, Tafadzwa Kutinyu, Steven Kingue na Hassan Mwasapili.

Maganga ameongeza kuwa Azam FC inawashukuru wachezaji hao, kwa mchango wao mkubwa walioutoa ndani ya Klabu hiyo na wana imani watafanya vizuri huko waendako.