Azam FC yajibu madai ya kuwa tawi la Simba

Jumatano , 20th Mei , 2020

Klabu ya Azam FC imekanusha vikali kauli za wadau wengi  na mashabiki wa soka nchini kuwa ina mahusiano na klabu ya Simba hasa katika masuala ya ndani ya uwanja.

Afisa Habari wake, Zakaria Thabit 'Zaka Zakazi'

Hayo yameelezwa na Afisa Habari wake, Zakaria Thabit 'Zaka Zakazi' alipokuwa katika mahojiano na Kipenga Xtra ya East Africa Radio, ambapo amesema kuwa habari hizo hazina ukweli na ni ukosefu  mkubwa wa heshima kwao.

Kumekuwepo na habari kwa mashabiki wengi wakiituhumu Azam FC kuwa inapendelea Simba kuliko Yanga na hata kudai kuwa katika mechi wanazokuta timu hizo, Azam imekuwa haioneshi ushindani mkali kwa Simba kama inavyoonesha kwa Yanga.

"Watu wanatukosea sana heshima, sisi si tawi la Simba na wala hatuna uhusiano wowote, wao wanaoongea hivyo watambue wanawakosea sana heshima wamiliki wa klabu ambao wamewekeza mabilioni ya pesa. Kama tungekuwa ni tawi lao basi tungewapa uwanja wetu", amesema Zaka Zakazi.

Mtazame zaidi hapa akieleza