Baada ya Yanga, Simba nayo yabadilishiwa ratiba

Jumatatu , 9th Sep , 2019

Ikiwa imepita siku moja tangu Bodi ya ligi ibadilishe ratiba ya Ligi Kuu kwa kuondoa mchezo namba 17 wa Yanga na Mbeya City, leo Septemba 9, 2019 Simba nayo imebadilishiwa ratiba yake.

Kikosi cha Simba

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, ratiba imebadilika kutokana na ratiba ya timu ya taifa kwa wachezaji wa ndani ambayo inashiriki kwenye mashindano ya CHAN na ratiba ya michuano hiyo ilichelewa kutoka.

Timu ya taifa ya Tanzania kwa wachezaji wa ndani, itaingia kambini Septemba 15 kuanza maandalizi ya kucheza na Sudan, Septemba 20 jijini Dar es salaam.

Athari hizo zimeukumbuka mchezo wa Simba dhidi ya Mtibwa Sugar ambao ulipangwa kuchezwa Septemba 18, 2019, hivyo umerudishwa nyuma na sasa utachezwa Ijumaa Septemba 13, 2019 saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.