Alhamisi , 12th Jan , 2017

Mkurugenzi Mkuu wa klabu Barcelona Oscar Grau amesema kuwa uwezo wa klabu hiyo kumpatia Lionel Messi kandarasi mpya yenye nyongeza ya mshahara itategemea uwezo wao wa kuvutia mapato kutoka kwa wadhamini na uuzaji wa wachezaji.

Lionel Messi

Kandarasi ya Messi inakamilika 2018 na anatarajia kupewa kandarasi mpya huku ikiripotiwa huenda akapewa kitita cha pauni milioni 21 wanazopata Luis Suarez na Neymar.

Ligi Kuu ya Hispania La Liga huweka mkataba na kila klabu kuhusu matumizi yao kila mwanzo wa msimu, ambapo huyazuia bodi kutotumia zaidi ya asilimia 70 ya bajeti yake ya mapato.

Kandarasi zenye mishahara mikubwa walizopatiwa Suarez na Neymar ambazo zitakamilika 2021, huchukua kiwango kikubwa cha matumizi ya timu hiyo.

Messi mwenye umri wa miaka 29, anaripotiwa kupokea pauni milioni 19 na Grau anasema kuwa nyongeza yoyote lazima ifikiriwe sana.