Bodi ya Wakurugenzi Simba yamteua Mwina Kaduguda

Jumatano , 20th Nov , 2019

Klabu ya soka ya Simba imemteua Mwina Kaduguda kuwa Kaimu Mwenyekiti wa klabu. Kaduguda anachukua nafasi hiyo kufuatia aliyekuwa Mwenyekiti Swedi Mkwabi kujiuzulu.

Moja ya vikao vya Bodi ya Wakurugenzi wa Simba.

Kwa mujibu wa taarifa ya Simba iliyotolewa leo Novemba 20, 2019, imeeleza kuwa uteuzi wa Kaduguda ambaye pia amewahi kuwa katibu mkuu wa Simba, umeanza jana Novemba 19, 2019.

Kwa upande mwingine Simba imemteua Salum Muhene kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo ambayo Mwenyekiti wa Bodi ni Mohammed Dewji.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa Bodi ya Wakurugenzi itatangaza tarehe ya uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti mpya wa klabu hapo baadaye.