Alhamisi , 6th Mei , 2021

Kiungo wa kati wa Manchester United Bruno Fernandes amesema kushinda kombe msimu huu kutaonyesha ishara ya kukua kwa kiwango cha Timu yao na jinsi inavyo endelea kuimarika kila siku.

Kiungo wa kati wa Manchester United Bruno Fernandes

United wanaingia katika mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali ya ligi ya uropa usiku wa leo Alhamis Mei 6, wakiwa na faida ya ushindi wa magoli 6 kwa 2 dhidi ya AS Roma walioupata katika mchezo wa mkondo wa kwanza katika dimba la Old Trafford wiki iliyopita. Fernandes mwenye umri wa miaka 26, hajacheza fainali yoyote akiwa na Man.Utd tangu ajiunge nayo mwezi Januari mwaka 2020.

Kiungo huyo wa kireno Ameongeza kusema kushinda taji tu bado haitoshi kwao lakini ni kitu kitakachokua watia moyo wachezaji na pia ni ishara kwamba wanafanya vizuri na kuendelea kujiboresha.