Jumamosi , 23rd Jun , 2018

Baada ya kufunga bao moja leo kwenye mchezo uliomalizika jioni hii kati ya Korea ya Kusini na Mexico, mshambuliaji wa timu ya taifa ya Mexico Javier Hernández ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa taifa hilo kufikisha mabao 50.

Javier Hernández (Chicharito), akishangilia baada ya kufunga bao.

Javier Hernández amefunga bao moja kwenye ushindi wa mabao 2-1 na kufikisha mabao 50 ya kuifungia timu ya taifa hivyo kuendelea kujikita kileleni mwa wapachika mabao wa taifa hilo.

Nyota huyo wa zamani wa Manchester United ambaye kwasasa anachezea West Ham United ya England yuko juu ya wachezaji Jared Borgetti (46), Hermosillo (35), Luis Hernández (35), Enrique Borja (31), Luis Roberto Alves (30).

Kwa upande mwingine Fainali hizi za Kombe la Dunia 2018 zimekuwa na rekodi ya kuwa na penati nyingi zaidi hadi sasa (14), kuliko za mwaka 2014 nchini Brazil ambapo zilipigwa penati 13 tu mpaka mashinadano yanamalizika.

Pia Mexico imeshinda mechi mbili mfululizo kwa amra ya kwanza kwenye Kombe la Dunia tangu ilipofanya hivyo kwa mara ya mwisho mwaka 2002 nchini Korea ya Kusini na Japan.