Jumatatu , 22nd Feb , 2016

Mabingwa watetezi wa michuano ya Coppa America Chile wamepangwa kundi moja na wapinzani wao katika fainali ya mwaka jana timu ya taifa ya Argentina ambapo wenyeji walifanikiwa kushinda kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Chile ambayo kwa mashindano ya mwaka huu hawatakua na kocha Jorge Sampaoli wameorodheshwa katika kundi D na timu za taifa za Bolivia,Argentina na Panama.

Mabingwa mara nyingi wa michuano hiyo Uruguay wapo Kundi C na timu za Venezuela, Jamaica na Mexico huku Brazil ikiangukia kundi B lenye timu za Peru, Haiti na Ecuador nalo kundi A likiundwa na timu za U.S.A, Paraguay, Costa Rica na Colombia.

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 03 mwaka huu ambapo Colombia itaumana na USA huko Santa Clara Calfornia.