Jumatano , 13th Feb , 2019

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Kangi Lugola amelitaka jeshi la polisi kwa kushirikiana na TCRA kuhakikisha mtu yoyote atakaye mtukana, kumdhihaki, ama kufanya uchochezi dhidi ya Rais Dkt John Magufuli achukuliwe hatua mara moja.

Rais John Magufuli

Akiongea leo ofisini kwake jijini Dar es salaam, Kangi amesema, "wanaomtukana Rais kuanzia sasa wasakwe popote pale walipo wakamatwe".

''Haiwezekani Rais akatukanwa, haiwezekani kabisa, iwe kwenye magroup ya WhatsApp, iwe kwenye ujumbe mfupi wa simu au blog na hata aina yoyote ya mawasiliano wachukuliwe hatua za kisheria'', amesisitiza.

Zaidi tazama video hapo chini akieleza vizuri.