Dilunga atoa siri ya ushindi wa Simba na goli lake

Jumanne , 30th Apr , 2019

Mfungaji pekee wa goli la ushindi leo kwenye mechi ya Ligi kuu kati ya Simba dhidi ya JKT Tanzania, Hassan Dilunga amesema walicheza kwa kushambulia muda wote wakijua watapata tu nafasi adimu.

Hassan Dilunga (katikati)

Akiongea mara baada ya mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa taifa na Simba kushinda goli 1-0 alilofunga mwenyewe, Dilunga ameweka wazi kuwa upana wa kikosi chao unawasaidia sana kushinda mechi.

''Tumecheza vizuri na ndio maana tumeshinda, kuumia kwa John Bocco halikuwa pengo kwetu sasa hivi kila mchezaji yupo vizuri tuna kikosi kipana kila mchezaji akipata nafasi anaonesha kiwango'', - amesema Dilunga.

Baada ya ushindi wa leo Simba sasa imefikisha pointi 72 ikiwa katika nafasi ya 2 nyuma ya Yanga yenye pointi 77 kileleni.

Simba sasa itasafiri kuelekea Mbeya ambako itacheza michezo miwili dhidi ya Mbeya City pamoja na Tanzania Prison kabla ya kurejea Dar es salaam.