Jumanne , 19th Mar , 2019

Klabu ya soka ya Yanga kupitia kwa msemaji wake Dismas Ten, imekemea vikali vitendo vinavyofanywa mitandaoni vya kupotosha ukweli kuhusu michango yao kutoka kwa wanachama.

Msemaji wa Yanga Dismas Ten

Dismas ameanza kwa kuinukuu moja ya taarifa inayosambaa mtandaoni inayosema kuwa yeye amewataka wanachama wa klabu hiyo wasitegemee timu kupata mafanikio kupitia michango yao.

''Kuna kurasa nyingi zimeanzishwa hasa 'Facebook' pia 'viblog' uchwara kujaribu kuvuruga mipango mizuri ya klabu yetu, jamaa zetu hawa wameanzisha utaratibu huu wakiamini watatuzuia kufikia malengo'', ameandika Dismas.

Dismas Ten amesema mpango huo wameshaujua na pamoja na wanaouendesha, akidai kuwa wengine ni waandishi kutoka kwenye vyombo vikubwa vya habari hivyo watawaanika muda wowote.

Yanga imeunda kamati maalumu ya kukusanya michango takribani kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwaajili ya matumizi mbalimbali ya klabu.