Alhamisi , 18th Oct , 2018

Kampuni ya Kwese Free Spors na EATV wameingia makubaliano ya kuonesha mbashara mechi za ligi kuu ya soka nchini Uingereza (EPL) kuanzia wikiendi hii, Oktoba 20.

Baadhi ya wachezaji wanaocheza ligi ya EPL

Makubaliano hayo yanahusisha kurusha  mchezo mmoja kila wikiendi ambapo wikiendi hii tunaanza na ‘Derby’ ya jiji la London kati ya West Ham United dhidi ya Tottenham Hotspurs, kuanzia saa 10:30 jioni.

Akizungumza kupitia kipindi cha Kipenga Xtra cha East Africa Radio, mkuu wa vipindi East Africa Radio, Nasser Kingu amesema, “ Kwanza tunawashukuru wasikilizaji wa Kipenga Xtra na Kipenga kwa  kutuunga mkono na kutambua hilo. Tunaendelea kuwaletea vitu vizuri kwaajili yao, Kwese Sports na EATV tumekubaliana kuonesha mbashara mechi za ligi kuu nchini Uingereza na tutaanza na Derby ya London kati ya West Ham United dhidi ya Tottenham Hortspurs”.

Kwahiyo tunawalika wapenzi wa kandanda kote nchini kujiunga na sisi katika uhondo huu wa ligi pendwa duniani. Hii si ya kukosa, mbashara kupitia EATV”, ameongeza.

Pia katika kuendeleza burudani ya ligi hiyo pendwa, Nasser Kingu amesema kuwa kila siku ya Jumatano, EATV itakuwa ikiwaletea watazamaji Highlights (marudio) ya jumla ya michezo yote iliyochezwa katika wiki husika.