Jumatatu , 21st Sep , 2020

Mlinda mlango, Essam El Hadary hafikirii kustaafu soka kwa sasa licha ya umri wake kufikia miaka 47,na kwa sasa anajiandaa kwa mazoezi ili aweze kujiunga na timu nyingine baada ya mkataba wake wa awali na Nogoom kumalizika .

Essam El Hadary akiwa katika moja ya mechi za timu yake ya Taifa.

El Hadary golikipa mzoefu ambaye amecheza soka la ushindani kwa zaidi ya miaka 25 mfululizo ,alitarajiwa kutangaza kustaafu mara baada ya msimu huu kumalizika  lakini amesema ataendelea kucheza

'' Umri wangu ni namba tu kwenye makaratasi,bado najiona nina nguvu za kucheza na kushindana  na vijana , Akizungumzia juu ya nafasi yake ya kuendelea kucheza soka, El Hadary amesema anafanya mazoezi kwa zaidi ya saa tatu  kila siku, ili kiwango chake kiendelee kuimarika kwa kuwa anaamini bado yupo imara tangu ashiriki kombe la dunia 2018 nchini Urusi.

Ikiwa atafanikiwa kupata timu na kujiunga nayo, huwenda akaingia katika vitabu vya kumbukumbu za kidunia kwa mchezaji kucheza akiwa na umri mkubwa japo kwa sasa inashikiliwa na Kazishoyi  Miura raia wa Japan anayecheza ligi kuu nchini humo akiwa na umri wa miaka 53.

Essam El Hadary katika maisha yake ya soka,ameichezea timu ya Taifa michezo zaidi ya michezo 150 kwa mafanikio makubwa ikiwemo kutwaa makombe manne ya  mataifa ya Africa (Afcon 1998 , 2006,2008 na  2010) tangu alipoanza kuitumikia timu ya Taifa mwaka 1996.

Vile vile El Hadary  alikuwepo katika  kikosi cha Misri kilichoshiriki kombe la dunia  2018 fainali zilizofanyikia nchini Urusi.

Kwenye ngazi za klabu, El Hadary  amevichezea vilabu vyote viwili vikubwa nchini  Misri kama  Al Ahly na Zamalek ambavyo ndio kioo halisi cha soka la nchi hiyo na Africa  kiujumla ambapo alifanikiwa kutwaa vikombe vingi tofauti na timu hizo.