Jumatano , 30th Sep , 2020

Patrice Evra amekiri kuwa na ubaguzi wa rangi katika timu ya Taifa ya Ufaransa, nahodha huyu wa zamani ambaye ameitumikia timu ya Taifa ya Ufaransa tangu mwaka 2004-2015 amelishutumu shirikisho la soka la Ufaransa kwa kufumbia macho jambo hili

Patrice Evra akiongea na vyombo vya habari

'' Nimelazimika  kumjibu Rais  wa Shirikisho la soka la Ufaransa Noel  Le Graet na kuueleza umma  juu  ukweli wa jambo hili, nina mifano  kadhaa juu ya ubaguzi wa wachezaji wenye asili ya Afrika tuliokuwemo katika timu ya Taifa''

'' Nakumbuka kuna siku Rais wa  nchi alitutembelea kambini, kuzungumza na wachezaji wa timu ya Taifa wakati wa kupiga picha ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu, pembeni ya Rais upande wa kushoto alikuwa  Mamadou  Sakho na  Bakar Sagna ambao wana asili ya Africa, lakini katika hali ya kushangaza  wachezaji hao waliondolewa na kuletwa  Hugo Lloris na Laurent Koscielny na Rais kusimama katikati yao'' anasema Evra

NI  KWELI KUNA UBAGUZI WA RANGI NDANI YA TIMU YA TAIFA  YA UFARANSA?

Ni dhana isiyoweza kuthibitishwa kwa urahisi,  kwa kuwa  historia inaonesha   mchanganyiko wa wachezaji wenye asili ya Afrika  katika kikosi cha timu ya Taifa ya Ufaransa umekuwepo tangu enzi hizo, wapo wachezaji waliocheza timu  hiyo kwa mafanikio makubwa  kama Jean Pierre Adam  1972-76 ambaye alizaliwa Senegal baadaye akaenda  Ufaransa,  Jean Pierre Tigana   1980-1988 alizaliwa Mali  na kwenda Ufaransa

Katika kikosi cha Ufaransa kilichotwaa ubingwa wa Dunia mwaka 1998  nyumbani Ufaransa kulikuwa na wachezaji  zaidi ya 10   katika timu hiyo akiwemo Patrick Viera, Marcel Desail, Thierry Henry Lilian Thuram   Zidane nk.Pia katika kikosi kilichotwaa ubingwa 2018 nchini  Urusi zaidi  ya wachezaji 10 wenye asili ya Africa walikuwemo akiwemo Paul Pogba,Ousman Dembele,Blaise Matuidi,Samwel Umutiti, Ng'olo Kante na wengineo