Jumanne , 12th Nov , 2019

Kiungo wa kati ya timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya Simba Jonas Mkude, ameondoka kwenye kambi ya timu ya taifa kwaajili ya kushughulikia mambo yake binafsi ya kifamilia.

Jonas Mkude

Taarifa ya Shirikisho la soka nchini (TFF), imeeleza kuwa kocha Mkuu wa kikosi hicho Ettiene Ndayiragije amempa ruhusa kiungo huyo.

Pia imeeleza kuwa kutokana na siku kubaki chache kuelekea mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2021 dhidi ya Equatorial Guinea, hatoongoza mchezaji wa kuziba nafasi ya Mkude.