Cristiano Ronaldo alifundisha na Sir Alex Ferguson kati ya mwaka 2003 hadi 2009.
Ronaldo alianzia benchi kama mchezaji wa akiba kwenye mchezo huo na baadae akaingia kipindi cha pili, jamba ambalo Ferguson anaamini iliwasaidia Everton kupata nguvu kwenye mchezo huo ambao ulichezwa katika dimba la Old Traford,
Kocha wa kikosi cha Manchester United Ole Gunnar Solskjaer aliweka wazi kuwa alifanya mabadiliko kwenye kikosi chake kilichoanza mchezo huo ikwemo Cristiano Ronaldo kuanza kama mchezaji wa akiba, ulikuwa ni mpango wake wa kumpumzisha baada ya kucheza mchezo mgumu wa ligi ya mabingwa dhidi ya Villarreal.
Sir Alex Ferguson ambaye alikinoa kikosi hicho cha mashetani hao wekundu kwa miaka 26 amenukuliwa kwenye moja ya vido iliyopostiwa mitandaoni akisikika akisema ari ya upambanaji ya Everton kwenye mchezo huo ilipanda baada ya kuona Ronaldo hajaanza katika mchezo huku akisistiza kuwa mara zote kocha unapaswa kuanza mchezo na wachezaji wako bora.
Rondlao mwenye unri wa miaka 36 na ni mchezaji bora wa Dunia mara tano ameshafunga mabao matano (5) kwenye michezo sita (6) tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Juventus katika dirisha la usajili lililopita.






