'First 11' ya Simba 2019/20 yawakosha mashabiki

Jumatano , 3rd Jul , 2019

Wakati usajili mbalimbali ukiwa unaendelea kwa klabu za Ligi Kuu Tanzania bara, mashabiki nao hawako nyuma kufuatilia kinachoendelea katika klabu zao.

Baadhi ya wachezaji waliosajiliwa na Simba

Usajili unaotikisa hivi sasa nchini n wa klabu kubwa za Simba, Yanga na Azam FC, huku Simba wakifanya kwa staili tofauti ya kutambulisha mchezaji kila siku za kazi, majira ya saa 7:00 mchana.

Leo imemtambulisha kiungo mshambuliaji, Ibrahim Ajib aliyekuwa akiwaniwa na TP Mazembe kutokea klabu ya Yanga kwa mkataba wa miaka miwili na kukifanya kikosi hicho kuwa cha moto kuelekea  msimu ujao wa ligi.

Kutana na shabiki kindakindaki wa klabu ya Simba, akitaja kikosi matata anachokiamini kuwa ni cha ushindi msimu ujao, msikilize hapa chini.