Ijumaa , 18th Jun , 2021

Dili ya kocha Ganaro Ivan Gattuso kujiunga na Tottenham Hotspurs imeyeyuka rasmi, baada ya mashabiki wa timu hiyo kumkataa kwa kauli mbiu (hashtag ) ya hapana kwa Gattuso katika mitandao ya kijamii.

Gattuso akimkaba koo kocha msaidizi wa Totternham Joel Jordan mwaka 2011

Mashabiki wa timu hiyo wamemkataa Gattuso kwa sababu ya kitendo chake alichokifanya miaka 10 iliyopita, akiwa nahodha AC Milan alipomkaba shingoni kocha msaidizi wa Tottenham wakati huo Joe Jordan katika mechi ya ligi ya mabingwa Ulaya katika hatua ya 16 bora katika uwanja wa San Siro mwaka 2011.

Gattuso alikuwa anatajwa kuchukua nafasi ya kocha Jose Mourinho aliyetimuliwa April 19 mwaka huu ndani ya kikosi cha Tottenham ,mkufunzi huyu ambaye ametoka kuachana na timu ya Fiorentina alikodumu kwa siku 23.

Tottenham wamekuwa wanatapatapa kusaka kocha mpya watakayefanya naye kazi kwa msimu ujao, awali walimtaja Antonio Conte kisha wakamgeukia Paulo Fonseca na baadaye Gattuso lakini hawajafanikiwa kwa wote watatu.