Jumamosi , 19th Jun , 2021

Timu ya taifa ya Ufaransa imebanwa mbavu na Hungary kwenye mchezo wa Kundi F’ kwenye muendelezo wa michuano ya Euro 2020, baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.

Antoine Griezmann

Kwenye mchezo ambao mabingwa wa Dunia Ufaransa walipewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi lakini walijikuta wanakibarua cha kutafuuta bao la kusawazisha baada ya Hungary kupata bao dakika ya 45 kupitia kwa mchezaji Attila Fiola. Lakini baadae kipindi cha pili kunako dakika ya 66 Antoine Griezmann akaifungia bao Ufaransa na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Sasa mabingwa hao wa Dunia wanafikisha alama 4 na ndio vinara wa kundi F’ wakati Hungary wapo nafasi ya 3 wakiwa na alama 1 walioipata leo.

Mchezo unaofata wa kundi F’ tutawashuhudia mabingwa mara tatu wa ulaya timu ya taifa ya Ujerumani wakiutafuta ushindi wa kwanza baada ya mchezo wa raundi ya kwanza kufungwa na Ufaransa kwa bao 1-0, hivyo wanahitaji ushindi au sare ili kufufua matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano hii, na wanakibarua kigumu mbele ya mabingwa watetezi Ureno ambao wao mchezo wa kwanza walishinda mabao 3-0 dhidi ya Hungary na ushindi kwa ureno utawahakikishia nafasi ya kusonga mbele hatua ya 16 bora. Mchezo huu utapigwa majara ya Saa 1:00 Usiku.

Na mchezo wa mwisho leo utachezwa Saa 4:00 Usiku ambao ni mchezo Pekee wa kundi E’ Hispania wataumana na timu ya taifa ya Poland. Hispania ina alama moja baada ya kutoka sare ya bila kufungana kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Sweeden, wakati Poland ilipoteza kwa kufungwa na Slovakia pkwa mabao 2-1.

Hispania ambao pia ni mabingwa mara tatu wa ulaya wapo kwenye presha kubwa kufuatia kiwango kilichoonyeshwa na safu yao ya ushambuliaji kwenye mchezo wa kwanza tofauti na matokeo ya ushindi hii leo itawaweka katika mazingira magumu ya kutinga hatua ya 16 bora.