'Hakuna mechi muhimu kama hizi mbili' - Kaseja

Jumatatu , 18th Nov , 2019

Golikipa wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya soka ya KMC, Juma Kaseja amesema kuwa wanaendelea kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mechi mbili za kwanza kuwania kufuzu AFCON 2021 kwani ndio zitatoa dira.

Juma Kaseja

Akiongea kutoka nchini Tunisia ambako Taifa Stars itacheza dhidi ya Libya kesho Jumanne Novemba 19, 2019, Kaseja amesema wanajiandaa vizuri na wachezaji wote wapo katika hali nzuri.

'Nilishasema kuwa michezo miwili hii ni ya muhimu sana kwetu, itatupa dira ya nafasi yetu katika kufuzu tena AFCON, hivyo watanzania waendelee kutuombea tu tufanye vizuri' - ameeleza.

Mchezo huo utapigwa kwenye mji wa Monastir,Tunisia kutokana na hali ya kiusalama nchini Libya kutokuwa vizuri.

Taifa Stars inashika nafasi ya pili kwenye kundi J ikiwa na pointi 3 sawa na vinara Tunisia lakini zikipishana idadi ya magoli ya kufunga.