Jumatatu , 12th Apr , 2021

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amemsifu mshambuliaji wake Edinson Cavani kwa kiwango bora alichoonyesha kwenye mchezo dhidi ya Tottenham na anaamini atamshawishi asalie klabu hapo, mkataba wa mshambuliaji huyo unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Edinson Cavani

Cavani alifunga bao la pili kwenye ushindi wa mabao 3-1 walioupata Manchester United dhidi ya Spurs kwenye mchezo wa ligi kuu. Bao hilo lilikuwa la 8 msimu huu katika michezo 29, licha ya kukosa michezo kadhaa kutokana na majeruhi na adhabu ya kukosa michezo.

Baada ya mchezo huo kocha wa kikosi hicho Ole Gunnar Solskjær alisema Cavani ameonyesha kiwango bora sana, na wanasubiri taarifa zake kama atasalia au ataondoka, na akasisitiza kuwa wamefungua mazungumzo ya wazi juu ya kuongeza mkataba na hakuna siri kuwa wanahitaji asalie klabu hapo.

Mshambuliaji huyo raia wa Uruguay mwenye umri wa miaka 34, alijiunga na Man United mwanzo mwa msimu huu na mkataba wake na mashateni wekundu unamalizaika mwishoni mwa msimu huu lakini kuna kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi endapo kama pande zote mbili zikikubaliana, na Amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu ya Boca Juniors ya Argentina.