Jumatano , 21st Oct , 2020

Mshambuliaji wa Manchester United Odion Ighalo amesema serikali ya Nigeria imetia aibu kufuatia ripoti kwamba wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji katika wilaya ya Lekki ya mji mkuu wa kibiashara Lagos siku ya Jumanne.

Mshambuliaji wa Manchester United na timu ya Taifa ya Nigeria akiwa katika majukumu ya nchi yake.

Wanigeria wamekuwa wakiandamana kila siku kwa karibu wiki mbili dhidi ya kitengo cha polisi, na Kikosi maalum cha kupambana na ujambazi ambacho vimeshutumiwa kwa miaka mingi kwa ulafi, unyanyasaji, mateso na mauaji.

Kupitia mtandao wake wa Twita Ighalo amesema''"Serikali ya Nigeria, mnatia aibu Ulimwenguni kwa kuua raia wenu mwenyewe, kutuma wanajeshi barabarani kuua waandamanaji wasio na silaha kwa sababu wanapigania haki zao?

"Ninyi watu mtakumbuka katika historia kama Serikali ya kwanza kutuma wanajeshi mjini kuanza kuua raia wao wenyewe. Ni aibu, tumechoka na nyinyi watu na hatuwezi kuvumilia".

Ighalo ameitaka Serikali ya Uingereza, viongozi wa ulimwengu na Umoja wa Mataifa kuingilia kati suala hili huku akisisitiza kwamba mauaji yataendelea iwapo Dunia itakaa kimya.