Jumanne , 17th Jul , 2018

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro leo amefungua kambi ya wanamichezo wa Polisi wanaojiandaa kushiriki michezo ya Shirikisho la Majeshi ya Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (EAPCCO GAMES 2018) inayotarajiwa kuanza Agosti 06 mwaka huu hapa nchini.

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro akiwa katika picha ya pamoja na wanamichezo wa timu ya Polisi na viongozi wengine wa Jeshi hilo wa nafasi za juu

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo uliofanyika katika Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga Jijini Dar es salaam, IGP Sirro amewataka wanamichezo hao kulinda heshima ya nchi kwa kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.

"Nawaomba mjiandae vizuri kuhakikisha mnaleta heshima nchini na jeshi la polisi kwa jumla, inaeleweka kwamba kuna zaidi ya polisi elfu 45, lakini nyinyi ndiyo mmechaguliwa kutuwakilisha, hivyo kafanyeni kweli", amesema IGP Sirro.

Pamoja na hayo, IGP Sirro ameendelea kwa kusema "hivi karibuni tu nilipoenda Uganda kwenye mkutano wa wakuu wa polisi, kila nchi ilikuwa inatamba itafanya kweli hivyo basi ili kudhihirisha sisi tupo vizuri, tunataka ushindi ubaki hapa nyumbani".

Baadhi ya michezo inayotarajiwa kuchezwa kwenye mashindano hayo ni pamoja soka, mpira wa mikono, volleyball, netiboli, ngumi, taekwondo, karate na kulenga shabaha, ipo katika Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, Jijini Dar es salaam.

Msikilize hapa chini IGP Simon Sirro akizungumza zaidi juu ya michuano hiyo