Jumamosi , 23rd Mar , 2019

Kiungo wa Simba James Kotei raia wa Ghana, amesema kwasasa ana undugu na Rais Magufuli na anaiunga mkono Taifa Stars huku akiwaomba msamaha wachezaji wenzake Emmanuel Okwi na Juuko Murushid ambao wanachezea Uganda.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kotei amesema amebatizwa na anaitwa James Magufuli kutoka Mwanza hivyo anashabikia Stars.

''Okwi na Juuko mtanisamehe mimi naitwa James Magufuli, kutoka Mwanza Tanzania, kesho nitashabikia Taifa Stars'' amendika James Kotei.

Kotei ambaye amekuwa kiungo tegemeo wa Simba, amejihami kuwa hakuna mtu aliyemwandikia ujumbe huo hivyo watu waamini kuwa ni yeye.