Alhamisi , 26th Mei , 2022

Jose Mourinho ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza barani ulaya kushinda makombe 3 tofauti ya vilabu barani ulaya baada ya kukiongoza kikosi cha AS Roma kutwaa ubingwa wa michuano ya Europe Conference League jana usiku.

Jose Mourinho akibusu kombe la Conference League

AS Roma chini ya Jose Mourinho wametwaa ubingwa wa Connference na kombe lao la kwanza kwenye michuano ya vilabu Ulaya kwa kuinyuka Feyenoord ya Uholanza kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali, bao pekee la mchezo huo limefungwa na Nicolo Zaniolo dakika ya 32.

Ubingwa huu umemfanya Mourinho kufikisha idadi ya makombe 5 ya vilabu barani ulaya aliyoshinda kama kocha. ameshinda ubingwa wa Klabu Bingwa (Uefa Champions League) mara 2 akiwa na FC Porto mwaka 2004, na Inter Milan 2010, pia ameshinda ubingwa wa Michuano ya UEFA Europa League mara mbili akiwa na FC Porto mwaka 2003 na 2017 akiwa na Manchester United. Hivyo ubingwa wa usiku wa jana ni wa 5 katika michuano 3 tofauti.

Mourinho pia hajapoteza mchezo hata mmoja wa fainali aliocheza kwenye michuano ya vilabu barani Ulaya katika fainali zote 5 alizocheza ameshinda zote. Na kombe hili ni la 26 kwa kocha huyo raia wa Ureno katika miaka yake 19 ya ukocha.