Julio aipa ukweli Simba, ataja inavyomnufaisha

Jumatatu , 10th Feb , 2020

Mchezaji wa zamani na aliyewahi kuwa kocha wa Simba, Jamhuri Kihwelo maarufu 'Julio' amesema kuwa klabu ya Simba ilikosea kumuondoa kocha Patrick Aussems wakati timu yake ilikuwa imeshajengeka.

Jamhuri Kihwelo Julio

Amesema hayo katika kipindi cha Kipenga Xtra kinachorushwa na East Africa Radio, wakati wa mjadala wa nini kinachoisumbua klabu ya Simba hivi sasa.

Julio amesema kocha yoyote anahitaji kupewa muda wa kutosha katika timu ndipo matunda yataanza kuonekana, akimtolea mfano kocha Aussems kuwa japo alifukuzwa lakini tayari alikuwa na kikosi bora na kilichotulia.

"Simba pale kuna tatizo kwa sababu mpaka tunamfukuza Uchebe tulikuwa tunaongoza ligi, hapo utasemaje?", amesema Julio.

Aidha Julio amefafanua kauli yake aliyoitoa hivi karibuni kuwa Simba ina wachezaji wazee, ambapo amesema hakumaanisha kuwa hawastahili kucheza lakini kuna mazingira wanashindwa kuendana nayo na kusisitiza kuwa yeye ni mzalendo wa timu hiyo na inamsaidia kwa mambo mengi.

Mtazame kwenye video hapa chini.